MRADI WA UMEME KV 33 MASASI WAFIKIA ASILIMIA 86

 



Na Mwandishi wetu

KAIMU Meneja Mkuu wa Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme nchini (ETDCO), Mhandisi Richard Mwanja amesema mradi wa ujenzi wa njia ya umeme wa kilovoti 33 kutoka Masasi kwenda Newala umefikia asilimia 86 ya utekelezaji, huku ukitarajiwa kukamilika ifikapo Mei 20, 2026.

Amesema ukamilikaji wa mradi huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza upatikanaji wa huduma ya umeme katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Akizungumza Mei 8,2026 Mkoani Mtwara wilayani ya Masasi, Kaimu Meneja huyo, Mhandisi Mwanja amesema mradi huo una urefu wa kilomita 76 na unahusisha ujenzi wa njia mpya ya umeme ambayo haijakatiza sehemu yoyote kutoka Masasi kuelekea Newala.

Amesema katika utekelezaji wa mradi huo jumla ya nguzo za zege 949 zinatakiwa kusimikwa, ambapo hadi sasa nguzo 914 tayari zimeshasimikwa.

"Huu ni mradi wa mwaka mmoja ambapo tuliingia site mwezi wa 10, hivyo tulitakiwa kumaliza mradi huu mwezi wa 10 mwaka huu," amesema.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA