RIO FERDINAND:"SIPO HAPA KWA AJILI YA SIASA, NIPO KUWAHAMASISHA VIJANA
NYOTA wa zamani wa Klabu ya Manchester United na timu ya Taifa ya Uingereza, Rio Ferdinand, amekanusha kuhusika na siasa wakati wa ziara yake nchini Tanzania, akisisitiza kuwa lengo lake kubwa ni kuhamasisha Vijana wenye vipaji na mapenzi kwenye soka.
Rio amesema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari, Mei 22, 2026 Jijini Dar es Salaam akiwa ameambatana na Mwenyeji wake, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda.
"Napenda kusisitiza kwamba mimi si mwanasiasa sipo hapa kuzungumzia siasa, sijawahi kufanya hivyo hata katika nchi yangu mwenyewe, na siwezi kufanya hivyo mahali pengine popote" alisisitiza Rio.
Ziara ya Rio imelenga kuimarisha maendeleo ya soka la vijana wa kitanzania kupitia taasisi yake iliyoko nchini Uingereza huku akiweka wazi dhamira yake ya kujenga akademia ya michezo hapa nchini.
Kwa upande wake Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Paul Makonda amesema, ndoto yake ilikuwa ni kumleta Mchezaji Rio Ferdinand asake vipaji vya Vijana wa Kitanzania kupitia Taasisi yake ili waende duniani na sio kupost ujio wake nchini kwenye mitandao ya kijamii.



Comments
Post a Comment